Friday, November 1, 2013

CHANZO CHA HARUFU MBAYA KINYWANI, JINSI YA KUEPUKA

Harufu mbaya mdomoni inachagizwa na mambo kadhaa ikiwamo tabia zetu za kila siku na maradhi ya meno.

Wakati mwingine jambo hili laweza kukufanya ushindwe kujiamini wakati wa kuzungumza na watu. Lakini pia laweza kuwafanya wanaokuzunguka wakushushe thamani wakidhani wewe ni mchafu...na kumbe una maradhi.

Tatizo la kunuka mdomo linawapata baadhi ya watu, ambao hata wakipiga mswaki, lakini bado ananuka mdomo hata pale anapotumia vitu vya kuufanya mdomo unukie vizuri kama ‘Chewing gum’ pipi hususan pipi-kifua na hata Big G bado mtu mwenye tatizo hilo ataendelea kuwa na harufu mbaya.

Wanasayansi wamekiri kwamba ni vigumu sana mtu kufahamu kuwa ana harufu mbaya kwa sababu ya mazoea lakini ni rahisi sana kutambua harufu kutoka kwenye kinywa cha mtu mwingine. Unaweza kutambua kama una harufu mbaya mdomoni kwa kumuuliza mtu unayemuamini na pia unaweza kujua harufu mbaya kwa kulamba nyuma ya kiganja na kunusa, wengine hupumua mbele ya kioo na kunusa.

Pia unaweza kutumia kijiti cha kuchokonolea meno na kukinusa. Kisayansi unaweza kutumia vifaa kama ‘Halimeter’, ‘Gas’ ‘Chromatography ‘na ‘BANA Test.

Daktari wa Kinywa wa Hospitali ya Kairuki Mikocheni jijini Dar es Salaam, Gillberth Lema anasema:

“Magonjwa ya kinywa yanasababishwa na mabaki ya chakula kwa kuwa mwili wa binadamu una vijidudu aina ya bacteria ambao kwa kitaalamu huitwa ‘normal flora’. Wadudu hao mara wanapokula hutoa tindikali ambayo husababisha magonjwa ya fizi na kinywa.

Vitu vyenye sukari ikiwemo sukari ya kawaida pia huchochea tatizo hili, lakini mpangilio wa meno katika kinywa huhifadhi mabaki na kuleta harufu mbaya,”

Anaeleza kuwa tatizo hili pia huchangiwa na vijidudu vya ‘bacteria’ wanaojificha kati ya jino na jino na wengine kama ana jino lililotoboka vijidudu hivi hutumia nafasi ya kujificha humo.

Lakini wale ambao wana tabia ya kulala mdomo wazi, tabaka la juu la ngozi ya mdomo huoza na kutoa harufu mbaya.

Unywaji Pombe: Unywaji wa pombe husababisha kiwango cha kabohaidreti kubaki mdomoni na kuoza hivyo kusababisha magonjwa ya fizi.

Chanzo kingine kikuu cha harufu mbaya ya kinywa ni pale ambapo chakula kingi kinabaki mdomoni hasa hasa nyama. Utumiaji wa chakula chochote kitakachokaa ndani ya mfumo wa usagaji wa chakula kwa muda mrefu kitaanza kuoza, na siku zote nyama inapooza huanza kutoa harufu mbaya ( kunuka ). Kwa hiyo hiki nacho ni chanzo kikubwa cha harufu mbaya ya kinywa.....

http://www.mwananchi.co.tz

No comments:

Post a Comment

PLEASE LEAVE YOUR COMMENTS HERE. HELP BLOG DEVELOPMENT

Print It: