Friday, November 1, 2013

NYUKI: TIBA YA GOUT NA UKIMWI



Baadhi ya wataalamu nchini wameanza kufanya utafiti juu ya tiba hii ya nyuki katika kutibu ‘gouts’.

Waswahili wanasema, mtaka cha uvunguni sharti ainame. Pia wanasema, anayependa waridi, basi avumulie miiba.

Vivyohivyo, hata katika tiba, wale wanaotaka uponyaji wamejikuta wakivumilia mambo mengi yanayoleta maumivu au kukera kama vile sindano na dawa. Hivyo, usishangae kuwa kuumwa na nyuki ikawa ni tiba tosha na thabiti kwako.

Wanasayansi wa Chuo Kikuu cha Tiba cha Washington, Marekani wanaeleza kuwa, sumu ya nyuki inaweza kuponya maradhi mbalimbali ikiwamo kuharibu virusi vya Ukimwi bila kuharibu seli za mwili wa binadamu.

Dk Joshua Hood, kiongozi wa utafiti huo anasema, ipo sumu kali iitwayo mellitin katika mwiba wa nyuki ambayo ina uwezo wa kuingia ndani ya mfuko unaozunguka kinga ya mwili wa binadamu na kuua virusi vya Ukimwi vilivyomo ndani.

Hata hivyo, imeelezwa kuwa sumu hiyo ya Mellitin iingiapo kwa wingi katika mwili wa binadamu, inaweza kuleta madhara.

Pia, Profesa Samule Wickline pia wa Marekani aliunda chembe ndogo zenye sumu ya mellitin, ambayo ina uwezo wa kuzuia saratani au dalili zozote z vivimbe vya saratani.

Hapa nchini, Dk Augustine Godman mtaalamu wa magonjwa ya uzeeni na mshauri wa kisaikolojia anasema amejaribu kutumia tiba ya nyuki kwa wagonjwa 158 wenye matatizo kwenye viungio vya mwili (gouts), ambayo husababishwa na wingi wa tindikali ya uric katika damu.

Anasema dawa hiyo imeonyesha matokeo mazuri kwa wagonjwa wengi ambao hung’atwa na nyuki katika sehemu mbalimbali za miili yao. Dk Godman anasema, yeye humuweka mgonjwa nje ilipo mizinga ya nyuki na kisha kuwafungulia wadudu hao kutoka katika mizinga yao.

Anasema nyuki wana sumu ambayo inaingia katika mwili wa binadamu na kuondoa sumu iliyo mwilini.

Wakati huohuo, Dk Hood anasema kuwa, sumu ya nyuki ina uwezo mkubwa wa kutoa tiba na kuunda mafuta ya uke ambayo yanaweza kuzuia maambukizi ya VVU na kuviua virusi sugu.

Watafiti hao wanaeleza kuwa sumu ya nyuki ina uwezo wa kuua wale askari wakubwa wanaofanya mashambulizi katika kinga ya mwili.

ENDELEA HAPA... http://www.mwananchi.co.tz/Nyuki--Mdudu-mkali-mwenye-sumu--aliyegeuka-tiba-duniani/-/1596774/2056274/-/e9v3svz/-/index.html

No comments:

Post a Comment

PLEASE LEAVE YOUR COMMENTS HERE. HELP BLOG DEVELOPMENT

Print It: