Saturday, January 4, 2014

MANYANYASO, UHUNI WA VIBAKA TENGERU ARUSHA KWA ABIRIANa Malisa Godlisten wa Facebook.

 Leo (Jana) nimeshuhudia mama tuliyekua nae kwenye gari moja, kutoka Moshi to (kwenda) Arusha akiporwa simu maeneo ya Tengeru na hakuna hatua iliyochukuliwa..
Baadhi ya abiria tulipojaribu kupaza sauti, wenzetu walionekana kutushangaa na kutuonya "hapa ni Tengeru, kama unajiamini shuka ufe."

Kisha kama utani vile, dereva akawasha gari safari ikaendelea.. mwizi ashatokomea kizani.. zogo likaanza ndani ya gari.. wengi walionekana kuwaogopa wezi wa Tengeru... na wengine wakawasifia eti "wanapasuaga hadi vioo vya gari majira ya usiku kama abiria aliyekaa dirishani ana kitu cha thamani.."

Huku mama wa watu akiwa ameduwaa kama amepata strock (mshituko) au anangojea hukumu pale The Heague (Mahakama ya kesi za kimataifa), zogo likaendelea... Konda akatuonya abiria eti kama wewe ni mgeni ukifika Tengeru ficha simu, hata ukipigiwa usipokee eti wanaweza kuondoka na sikio..

Nimekasirika sana, nimefadhaika sana, nimeumia sana.. Hivi nchi hii tumefikia hatua ya kutukuza vibaka kiasi hiki?? Hivi Jeshi la Polisi wanafahamu vibaka wa Tengeru wanavyoogopwa?

Sidhani kama nimewahi kufadhaika kwa kiasi hiki cha leo.. unipore mali yangu, niliyotafuta kwa jasho langu... halafu uonekane mbabe??.. yeleuwi nakufuata.!!!

Kwangu mm kibaka ni kibaka tu.. awe wa Tengeru, Nyegezi au Kariakoo.. Sasa iweje hawa wa Tengeru waonekane VIP?? Hivi Arusha hamna matairi?? Kwnn msiwageuze wawili kuwa ndafu,.ili iwe fundisho kwa wengine.??

Najaribu tu kuwaza kwa hasira..!!!


Kufuatia tukio la jana la mama aliyeporwa simu kwenye gari maeneo ya Tengeru, nimempigia sinu RPC wa Arusha ACP Liberatus Sabas kupitia simu yake ya mkononi namba 0713 269 232, lakini haikupokelewa..
Hivyo nimemuandikia ujumbe wa maandishi (sms) kumjulisha juu ya tukio la jana, na kumshauri mambo yafuatayo:

1.Aimarishe ulinzi maeneo ya Tengeru ikiwa ni pamoja na kuweka doria hasa maeneo ya usiku.

2.Kwa kuwa eneo la Tengeru limeonekana kuwa hatari kwa usalama wa watu na mali zao, na kwa kuwa vitendo vya uhalifu vimeonekana kuwa sugu, ni muda muafaka sasa, jeshi la Polisi kufikiria Tengeru kuwa wilaya maalum ya kipolisi, itakayohudumia maeneo ya Tengeru, USA, Nduruma, Kilala, Nkoaranga na maeneo jirani..!!

Kama Kimara, ambalo ni eneo dogo na lisilo na uhalifu wa kutisha kama huu wa Tengeru, limefanywa wilaya maalumu ya kipolisi, naamini Tengeru haitashindikana.

3.Kwa kuwa askari polisi wa Tengeru na maeneo jirani wanatuhumiwa kulinda wahalifu, ni vema kamanda Sabas akawahamisha Askari wote wa maeneo ya Tengeru na vituo jirani ili kupima ukweli wa tuhuma hizo.

Akiweka askari wapya baada ya muda atabaini kama tuhuma hizi ni za kweli au lah.!

4.Kwa kuwa inadaiwa uhalifu huu unafanywa na wazawa, ni vema ulinzi shirikishi ukaimarishwa.. Wapo wazawa ambao ni raia wema, so naamini wakishirikishwa vema kwny zoezi la ulinzi, wanaweza kuwataja wanaohatarisha amani maeneo hayo na wakachukuliwa hatua.

5.Kwa kuwa madereva na makonda wa gari za Arusha Moshi nao wanatuhumiwa kufanya kazi na vibaka, ni vema ukaguzi wa mara kwa mara ukafanyika ili kujiridhisha na madereva hao.. Si ajabu baadhi ya vibaka wanaachiwa magari kupiga deiwaka hivyo wanajua nani mwenye simu "kali" wamzungukie badae.!!


TOA MAONI YAKO> SAIDIA KUTOKOMEZA UHALIFU

No comments:

Post a Comment

PLEASE LEAVE YOUR COMMENTS HERE. HELP BLOG DEVELOPMENT

Print It: