This Blog is created to provide Multi-information Including What Ever is Out There For You
LIKE ME ON FACEBOOK
Popular Posts
Useful Links
Showing posts with label TANZANIA. Show all posts
Showing posts with label TANZANIA. Show all posts
Saturday, January 4, 2014
MANYANYASO, UHUNI WA VIBAKA TENGERU ARUSHA KWA ABIRIA
Na Malisa Godlisten wa Facebook.
Leo (Jana) nimeshuhudia mama tuliyekua nae kwenye gari moja, kutoka Moshi to (kwenda) Arusha akiporwa simu maeneo ya Tengeru na hakuna hatua iliyochukuliwa..
Baadhi ya abiria tulipojaribu kupaza sauti, wenzetu walionekana kutushangaa na kutuonya "hapa ni Tengeru, kama unajiamini shuka ufe."
Kisha kama utani vile, dereva akawasha gari safari ikaendelea.. mwizi ashatokomea kizani.. zogo likaanza ndani ya gari.. wengi walionekana kuwaogopa wezi wa Tengeru... na wengine wakawasifia eti "wanapasuaga hadi vioo vya gari majira ya usiku kama abiria aliyekaa dirishani ana kitu cha thamani.."
Huku mama wa watu akiwa ameduwaa kama amepata strock (mshituko) au anangojea hukumu pale The Heague (Mahakama ya kesi za kimataifa), zogo likaendelea... Konda akatuonya abiria eti kama wewe ni mgeni ukifika Tengeru ficha simu, hata ukipigiwa usipokee eti wanaweza kuondoka na sikio..
Nimekasirika sana, nimefadhaika sana, nimeumia sana.. Hivi nchi hii tumefikia hatua ya kutukuza vibaka kiasi hiki?? Hivi Jeshi la Polisi wanafahamu vibaka wa Tengeru wanavyoogopwa?
Sidhani kama nimewahi kufadhaika kwa kiasi hiki cha leo.. unipore mali yangu, niliyotafuta kwa jasho langu... halafu uonekane mbabe??.. yeleuwi nakufuata.!!!
Kwangu mm kibaka ni kibaka tu.. awe wa Tengeru, Nyegezi au Kariakoo.. Sasa iweje hawa wa Tengeru waonekane VIP?? Hivi Arusha hamna matairi?? Kwnn msiwageuze wawili kuwa ndafu,.ili iwe fundisho kwa wengine.??
Najaribu tu kuwaza kwa hasira..!!!
Kufuatia tukio la jana la mama aliyeporwa simu kwenye gari maeneo ya Tengeru, nimempigia sinu RPC wa Arusha ACP Liberatus Sabas kupitia simu yake ya mkononi namba 0713 269 232, lakini haikupokelewa..
Hivyo nimemuandikia ujumbe wa maandishi (sms) kumjulisha juu ya tukio la jana, na kumshauri mambo yafuatayo:
1.Aimarishe ulinzi maeneo ya Tengeru ikiwa ni pamoja na kuweka doria hasa maeneo ya usiku.
2.Kwa kuwa eneo la Tengeru limeonekana kuwa hatari kwa usalama wa watu na mali zao, na kwa kuwa vitendo vya uhalifu vimeonekana kuwa sugu, ni muda muafaka sasa, jeshi la Polisi kufikiria Tengeru kuwa wilaya maalum ya kipolisi, itakayohudumia maeneo ya Tengeru, USA, Nduruma, Kilala, Nkoaranga na maeneo jirani..!!
Kama Kimara, ambalo ni eneo dogo na lisilo na uhalifu wa kutisha kama huu wa Tengeru, limefanywa wilaya maalumu ya kipolisi, naamini Tengeru haitashindikana.
3.Kwa kuwa askari polisi wa Tengeru na maeneo jirani wanatuhumiwa kulinda wahalifu, ni vema kamanda Sabas akawahamisha Askari wote wa maeneo ya Tengeru na vituo jirani ili kupima ukweli wa tuhuma hizo.
Akiweka askari wapya baada ya muda atabaini kama tuhuma hizi ni za kweli au lah.!
4.Kwa kuwa inadaiwa uhalifu huu unafanywa na wazawa, ni vema ulinzi shirikishi ukaimarishwa.. Wapo wazawa ambao ni raia wema, so naamini wakishirikishwa vema kwny zoezi la ulinzi, wanaweza kuwataja wanaohatarisha amani maeneo hayo na wakachukuliwa hatua.
5.Kwa kuwa madereva na makonda wa gari za Arusha Moshi nao wanatuhumiwa kufanya kazi na vibaka, ni vema ukaguzi wa mara kwa mara ukafanyika ili kujiridhisha na madereva hao.. Si ajabu baadhi ya vibaka wanaachiwa magari kupiga deiwaka hivyo wanajua nani mwenye simu "kali" wamzungukie badae.!!
TOA MAONI YAKO> SAIDIA KUTOKOMEZA UHALIFU
Labels:
TANZANIA
Thursday, January 2, 2014
HOTUBA YA RAISI KIKWETE, UJENZI WA MIUNDO MBINU NA NISHATI
SALAMU
ZA MWAKA MPYA ZA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHESHIMIWA DKT. JAKAYA
MRISHO KIKWETE KWA WATANZANIA,
TAREHE
31 DESEMBA, 2013
CONTINUED
Ujenzi
wa Miundombinu
Ndugu wananchi;
Katika
mwaka 2013, tumeendelea kupata mafanikio makubwa katika kuboresha miundombinu
ya usafiri wa ardhini, majini na angani. Kasi ya ujenzi wa barabara imeendelea
kufanyika kote nchini. Kazi ya ujenzi ingekuwa nzuri zaidi kama mtiririko wa malipo
kwa Wakandarasi ungekuwa mzuri. Tatizo hili
tutalitafutia ufumbuzi mwaka 2014 ili kasi ya ujenzi wa barabara za lami nchini
iwe nzuri zaidi.
Pamoja na hayo mwaka
huu kilomita 877 za barabara
zimekamilika. Ujenzi wa daraja la Malagarasi nao umekamilika kinachosubiriwa ni
sherehe za uzinduzi. Ujenzi wa daraja la Kilombero umeanza na ule wa daraja la
Kigamboni unaendelea vizuri. Tunatarajia kuwa mwakani tutaongeza zaidi kasi ya
ujenzi wa barabara zilizosalia ikiwa ni pamoja na kujenga baadhi ya barabara
kwa ubia na sekta binafsi. Kwa kasi na
mwenendo tunaoendelea nao sasa naamini ifikapo mwaka 2015 tutakuwa tumefikia
hatua ya juu sana katika shabaha yetu ya kuunganisha mikoa yote nchini kwa
barabara za lami.
Ndugu Wananchi;
Jitihada
za kupunguza msongamano wa magari katika Jiji la Dar es Salaam zimeendelea kutekelezwa. Barabara kadhaa zilipanuliwa na kazi
inaendelea. Ujenzi wa njia ya kupita
mabasi yaendayo haraka umeendelea kwa kasi ya kuridhisha. Mchakato wa ujenzi wa barabara za juu ya
nyingine katika njia panda za TAZARA na Ubungo umeshaanza. Mwaka ujao huduma ya usafiri wa treni kusafirisha
abiria Dar es Salaam itaongezwa ili watu wengi zaidi wanufaike.
Ndugu wananchi;
Mwaka
huu, kwa upande wa reli ya kati, kazi ya kuboresha njia ya reli imeendelea
kufanyika na itaendelea mwaka 2014. Mwakani
(2014) Shirika la Reli litapokea injini mpya 13, mabehewa ya mizigo 274
na breki 34 hivyo kuboresha sana
huduma katika reli ya kati. Kuhusu
ujenzi wa reli mpya ya upana wa kimataifa ni matarajio yetu kuwa kama kila kitu
kitaenda sawa mchakato wa ujenzi utaanza katika nusu ya pili ya mwaka 2014.
Ndugu Wananchi;
Tumetoa kipaumbele
cha juu katika kuboresha huduma ya usafiri wa anga nchini. Mwaka huu, tumeendelea na ukarabati, upanuzi
na ujenzi wa viwanja vya ndege vya Mikoa ya Kilimanjaro, Kigoma, Tabora,
Mwanza, Arusha, Mtwara na Kagera. Ni
jambo la kufurahisha kuona Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe ukianza
kutumika. Hatimaye ndoto imetimia. Mwaka
wa 2014 ujenzi wa majengo mengine ya kuhudumia abiria, mizigo na ndege utaendelea
katika uwanja huo.
Pia ni furaha iliyoje
kwamba upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Mafia na ujenzi wa gati la Kilindoni vimekamilika. Kero ya miaka mingi imepatiwa ufumbuzi. Kazi ya ujenzi wa jengo jipya la abiria
katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere itaanza rasmi mwaka 2014.
Nishati
Ndugu wananchi;
Dhamira
yetu ya kutaka Tanzania iwe na umeme wa uhakika na unaonufaisha watu wengi
imepata sura na mwelekeo mzuri mwaka huu 2013.
Ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara na Songosongo kuja Dar es Salaam
umeanza na utekelezaji unakwenda vizuri.
Kama ujenzi wa bomba utakamilika kama inavyotarajiwa na ujenzi wa
mitambo ya kuzalisha umeme Kinyerezi utaenda kama ilivyopangwa, ifikapo mwaka
2015 Tanzania itafikia lengo la kuzalisha megawati
3,000 za umeme.
Ndugu Wananchi;
Bahati nzuri mwaka
huu, kufuatia kuongezewa fedha za bajeti, kasi ya usambazaji umeme imekuwa
nzuri. Tunaumaliza mwaka huku idadi ya
Watanzania waliounganishiwa umeme ikiwa imefikia asilimia 24 ukilinganisha na asilimia
21 mwaka 2012 na asilimia 10
mwaka 2005. Haya si mafanikio madogo. Kwa mwelekeo huu, kufikia lengo la asilimia 30 ya Watanzania kupata umeme mwaka
2015 ni jambo la uhakika kabisa sasa. Tena kuna uwezekano mkubwa wa kulivuka
lengo hilo.
Endelea USHIRIKIANO WA KANDA NA EAC
Endelea USHIRIKIANO WA KANDA NA EAC
Labels:
TANZANIA
Subscribe to:
Posts (Atom)

